loader
Mbunge alia na ubovu viwanja vya michezo

Mbunge alia na ubovu viwanja vya michezo

Mbunge wa Jimbo la Makete mkoani Njombe, Festo Sanga ameendelea kupaza sauti juu ya ubovu wa viwanja vya mpira wa miguu nchini.

Akiuliza swali la nyongeza leo Mei 24, 2022 bungeni jijini Dodoma, Sanga amesema: " Ni mwaka mmoja sasa tangu Rais Samia Suluhu Hassan atoe maelekezo kwa wizara na Chama cha Mapinduzi kuanza kuboresha viwanja nchini hasa eneo la kuchezea, lakini, tangu Rais aseme kumekuwa kimya, ni upi mkakati wa serikali kuboresha viwanja hivyo?.

Akikazia swali hilo, Naibu Spika, Mussa Azzan Zungu amesema: "Hata Yanga jana imeshindwa kucheza vizuri pale Mwanza kutokana na uwanja mbovu".

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul amesema: "Serikali inaendelea na majadiliano na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuanza matengenezo kwa viwanja saba na fedha zimeanza kutengwa kwenye bajeti ya mwaka huu."

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7c646358b6b53a26e6a64c11a89118eb.png

RAIS Samia Suluhu Hassan, amewapongeza wachezaji ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi