loader
Mtandao wa matapeli wa viwanja wanaswa

Mtandao wa matapeli wa viwanja wanaswa

POLISI  mkoani Morogoro inawashikilia watu 16 kwa tuhumza za kujihusisha na utapeli wa kuuza viwanja kwa mtu zaidi ya mmoja wakitumia  nyaraka za kugushi  na kugonga mihuli bandia  ili kutekeleza uhalifu wao na kujipatia mamilioni ya fedha .

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo ,Fortunatus Musilimu amesema  hayo leo Mei 25, 2022  wakati akizungumza na waandishi wa habari ya kwamba watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti kuanzia jana Mei 24, 2022.

Amesema  watuhumiwa hao wamekuwa wakishirikiana na viongozi mbalimbali wasiowaadilifu wa maeneo husika kupima viwanja katika mashamba yasiyokuwa yao, kuandaa mihtasari feki  na hati bandia za umiliki na uuzaji wa viwanja na mashamba hayo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo amesema, watuhumiwa hao wamekuwa wakishirikiana na watendaji wa Taasisi, Mamlaka, na Idara mbalimbali za serikali katika kutenda uhalifu huo.

Amesema   watuhumiwa hao wamekuwa kero na kuzua taharuki katika jamii na kusababisha kutokea kwa uvunjifu wa amani  na wamekuwa wakishirikiana na wahalifu wenzao kutoka nje ya mkoa wa Morogoro kufanya  uhalifu  huo na kuondoka.

Musilimu ametoa angalizo kwa kuwataka wote wanaojihusisha na utapeli wa viwanja na mashamba mkoani Morogoro kuacha mara moja  kwani hawatakuwa salama.

“ Wote waliojihusisha katika utapeli wa viwanja na kutoroka au kuhama wajue kwamba watatafutwa huko walipo na kutiwa mbaroni na kurejeshwa kujibu tuhuma zao …ni vyema wakajisalimisha wenyewe badala ya kusubiri kutafutwa” ameonya   Kamanda Musilimu

Amesema kuwa Polisi itaendelea kuhojiana nao ili kubaini mtandao mzima  na hivyo  kuwataka wote ambao waliwahi kutapeliwa viwanja vyao kufika Kituo cha Polisi cha Kati (Central Morogoro)  ili kuwatambua watuhumiwa hao kwa hatua za kisheria.

Musilimu amesema  ,wale wote ambao kesi zao zipo Mabaraza ya Ardhi  na Mahakamani ambao wametapeliwa na watuhimiwa hao kufika kuwatambua  na hata wale wote ambao walitapeliwa na kukosa haki  na kusamehe kwa kumuachia Mungu wafike ili wapate haki yao.

“ Hakuna tapeli atakayeachwa , kila jiwe litaguswa “ meonya  Kamanda  Musilimu

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7ba7b3f0a29bbb123420d78e21836718.jpg

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mradi wa ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi