loader
Tamisemi kinara malalamiko  Takukuru

Tamisemi kinara malalamiko Takukuru

OFISI ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), imetajwa kuwa kinara wa kulalamikiwa katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) .

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Takukuru wa Mkoa wa Katavi, Festo Mdede,   leo Mei 25 Mwaka huu.

Amesema jumla ya malalamiko 58  yaliwasilishwa  kuanzia Januari mpaka Machi Mwaka huu.

Amesema mbali na Tamisemi pia Idara au Sekta ambazo kila moja imelalamikiwa mara moja zimetajwa ni Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA),  Kilimo, Madini, Dini na Bima.

Idara au Sekta nyingine na idadi ya malalamiko dhidi yake katika mabano zimetajwa ni Mahakama (15), Elimu (14), Ardhi (13), Afya (12), fedha (6) Polisi (6), Tanesco (3), Binafsi (3) na Ushirika (2 ).

"Katika kipindi hiki cha miezi mitatu, tumepokea jumla ya malalamiko 139,  kati ya hayo 106 yanahusu  rushwa, 33 hayakuhusu rushwa." Amesema Mdede

Amesema wahusika wa malalamiko yasiyohusu rushwa walielimishwa na kushauriwa huku malalamiko yanayohusu rushwa yakifunguliwa majalada ya uchunguzi, yanafanyiwa.

foto
Mwandishi: Swaum Katambo, Katavi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi