loader
Wanafunzi wa elimu ya kati, wafikiriwa mikopo

Wanafunzi wa elimu ya kati, wafikiriwa mikopo

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea kufanya tathmini ya taarifa ya tume iliyoundwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ili iangalie namna ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ngazi ya kati.

Amesema hayo wakati akiweka jiwe la msingi kwenye jengo la Ufundi Tower katika Chuo cha Ufundi Arusha na kumuagiza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ahakikishe anasimamia ujenzi huo ili wanafunzi wa chuo hicho waweze kulitumia jengo hilo.

“Wabunge waliishauri Serikali kuwa tuangalie ni namna gani tunaweza kuwawezesha wanafunzi wa ngazi ya kati ya astashahada na cheti, kada ambayo ndiyo yenye wataalaamu wanaoingia field, sasa tumeona tuimarishe na tutalifanyia kazi.”Amesema Majaliwa

 Amesema kuwa katika bajeti ya mwaka huu Serikali itaendelea kuhakikisha kila mwanafunzi anayetoka katika familia zisizokuwa na uwezo wa kujilipia gharama mbalimbali kwenye vyuo ananufaika na mikopo hiyo. “Maboresho mbalimbali katika sekta ya elimu nchini yanaendelea”

Awali, Waziri Mkuu alitembelea eneo la Njiro inakojengwa hospitali ya Wilaya ya Arusha ili kukagua ujenzi wa majengo ya idara ya wagonjwa wa nje (OPD) ambayo yanatarajiwa kugharimu sh. bilioni 3.91.

 Waziri Mkuu amemtaka mkandarasi anayejenga hospitali hiyo kutoka kampuni ya Ladwa ahakikishe anakamilisha kazi hiyo ifikapo Septemba, mwaka huu kama alivyoahidi.

“Wananchi hawa wanatarajia kazi hii ikienda kwa mfululizo, wajibu wetu ni kuwahakikisha kwamba kazi hii inakwenda, mkandarasi tumeshakupa fedha, tunatarajia kila siku utakuwa hapa.”

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi