loader
NECTA  yafafanua faida  usahihishaji kidijiti

NECTA yafafanua faida usahihishaji kidijiti

BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) limepanga kusahihisha mitihani ya taifa na ile ya upimaji wa kitaifa kwa mfumo wa kidijiti.

Hatua hiyo italiwezesha baraza kuokoa Sh bilioni 30 zilizokuwa zikitumika kwa kazi hiyo kila mwaka. Hayo yamebainishwa na Ofisa Uhusiano wa NECTA, John Nchimbi alipozungumza na HabariLEO mwishoni mwa wiki wakati wa Wiki ya Ubunifu iliyoenda sambamba na Maonesho ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU).

Alisema katika kutekeleza hilo, baraza lilianza kutumia mfumo huo mwaka jana kusahihisha mtihani wa taifa wa kuhitimu elimu ya msingi.

Nchimbi alisema pia kwa mwaka huu, baraza litatumia mfumo wa kusahihisha kidijiti kwa mitihani ya ualimu hatua ambayo itaokoa takribani Sh milioni 500.

“Mwaka jana tumeanza na mitihani ya darasa la saba, mwaka huu tutasahihisha mitihani ya walimu na mwaka 2023, tutahamia kwenye mitihani ya kidato cha sita, mwaka 2024 tutasahihisha ile ya upimaji wa kitaifa wa darasa la nne na kidato cha pili na mwaka 2025 itasahihisha ile ya kidato cha nne na upimaji wa maarifa,” alisema.

Nchimbi alisema kama ilivyo utaratibu wa sasa, msahihishaji atapewa kusahihisha swali moja pekee huku akiwa kwenye kompyuta yake katika kituo chake cha kazi.

Alisema baraza litabadili mtihani kuwa kwenye mfumo wa kikompyuta na kupitia mfumo swali husika ndio litakwenda kwa msahihishaji.

“Mfumo unampa fursa msahihishaji kusoma swali husika, kuangalia mwongozo wa usahihishaji na baadaye kusahihisha kulingana na mwongozo huo, akishamaliza kusoma swali hata kama lilikuwa la kujieleza, kazi hiyo itakwenda kwa mhakiki kuangalia kama msahihishaji amefanya kazi yake vizuri.”

“Kama mhakiki anaona mwanafunzi hakutendewa haki, atatoa maoni na kuyarejesha kwa anayesahihisha na kama anaona yuko sahihi basi mtihani huo wa mwanafunzi utapelekwa kwa kiongozi kwa ajili ya kufanywa uamuzi,” alisema.

Nchimbi alisema mbali na faida ya kupunguza gharama, mfumo huo pia unasaidia katika kujumlisha alama ambazo msahihishaji amezitoa hivyo kuondoa makosa ya kibinadamu katika hilo

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7d292a0c4d4cf7fc20b32d5ebd3601a2.jpg

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mradi wa ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi