loader
Waamuzi Simba, Yanga watajwa

Waamuzi Simba, Yanga watajwa

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetaja waamuzi na maofi sa watakaosimamia michezo miwili ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam, itakayochezwa Mei 28 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza pamoja na Mei 29 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

Mchezo wa Jumamosi kati ya Simba na Yanga, mwamuzi wa kati atakuwa Ahmed Arajiga (Manyara), msaidizi namba moja ni Frank Komba (Dar es Salaam), namba mbili atakuwa Mohamed Mkono (Tanga), mwamuzi wa akiba atakuwa Elly Sasii (Dar es Salaam) na Mtathmini wa waamuzi ni Victor Mwandike (Mtwara).

Kamishna wa mchezo ni Keneth Pesambili (Katavi), Mratibu wa mchezo, Baraka Kizuguto (Dar es Salaam), Mratibu msaidizi, Ibrahim Mohamed (Dar es Salaam), Ofisa Itifaki, Jackline Kamwamu (Dar es Salaam), Ofisa Masoko, Aron Nyanda (Dar es Salaam), Ofisa Habari, Cliford Ndimbo (Dar es Salaam) na Ofisa Usalama ASP Hashim Abdallah (Dodoma).

Katika mchezo wa nusu fainali wa pili kati ya Azam FC na Coastal Union, mwamuzi wa kati atakuwa Ramadhani Kayoko kutoka Dar es Salaam, mwamuzi msaidizi namba moja, Ferdinand Chacha (Mwanza), namba mbili akiwa Soud Lila (Dar es Salaam), Mwamuzi wa akiba, Kasim Mpanga (Dar es Salaam).

Mtathmini wa waamuzi atakuwa Emmanuel Chaula (Katavi), Kamishna wa mchezo ni Blassy Kiondo (Rukwa), Mratibu wa mchezo, Kassim Haji (Dar es Salaam), Ofisa Itifaki, Irene Benard (Dar es Salaam), Ofisa Masoko, Fredrick Masolwa (Dar es Salaam) na Ofisa Habari, Hakim Mikidadi (Dar es Salaam).

Wakati huohuo, Ofisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo amesema kuwa maandalizi ya pambano la Yanga na Simba litakalofanyika Jumamosi yamekamilika, kila kitu kiko vizuri. Alisema viingilio vya mchezo huo ni mzunguko Sh 10,000, VIP Sh 20,000 na VIP A ni Sh 30,000.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5634939cd3d9f93e47bd161e1688a322.jpeg

RAIS Samia Suluhu Hassan, amewapongeza wachezaji ...

foto
Mwandishi: Waandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi