loader
Klopp kocha bora wa mwaka

Klopp kocha bora wa mwaka

CHAMA cha Makocha wa Ligi Kuu England kimemtangaza Jurgen Klopp wa Liverpool kuwa kocha bora wa mwaka.

Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 54, ametwaa taji la Sir Alex Ferguson, baada ya kupigiwa kura na makocha wanachama wa ligi za madaraja yote.

Klopp pia alishinda tuzo ya meneja bora wa Ligi Kuu licha ya kikosi chake kukosa taji baada ya kumaliza ligi kikiwa pointi moja nyuma ya Manchester City Jumapili.

Kocha wa Chelsea, Emma Hayes alishinda tuzo ya kocha bora wa Ligi ya Wanawake. Chelsea ilishinda kwa mara ya tatu mfululizo taji hilo mapema mwezi huu, baada ya kuifunga Manchester City 3-2 katika fainali ya Kombe la FA.

Liverpool ya Klopp ilikuwa tayari imeshashinda Kombe la FA na lile la Ligi msimu huu na timu hiyo inakutana na Real Madrid katika fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya Jumamosi.

Katika orodha ya kuwania tuzo hiyo alikuwepo Kocha wa Man City, Pep Guardiola, yule wa Brentford, Thomas Frank, wa Newcastle, Eddie Howe na wa Crystal Palace, Patrick Vieira.

“Ni heshima kubwa na ulikuwa msimu wa aina yake,” alisema Klopp. “Hayakuwa matokeo mazuri kwetu, lakini tumeyamaliza.” Kocha huyo aliongeza: “Unaposhinda tuzo kama hii ni ama ni mtu mwenye akili nyingi au una benchi zuri la ufundi duniani na niko hapa na benchi langu lote la ufundi, wanajua jinsi ninavyowakubali wao.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f083b79e9a36054da281de0b742cb8d7.jpg

Klabu ya soka ya Chelsea imefikia muafaka ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi