loader
Geita waelezwa umuhimu wa kujisajili VAT

Geita waelezwa umuhimu wa kujisajili VAT

MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) Mkoa wa Geita, imewataka wafanyabiashara kuondoa dhana potofu juu ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), badala yake wanapokidhi vigezo wasajiliwe, ili kupata fursa za kiuchumi.

Kauli hiyo inakuja baada ya kubainika baadhi ya wafanyabiashara waliotimiza vigezo wamekuwa hawana uelewa juu ya VAT na kukwepa kusajiliwa pasipo kujua kodi hiyo inalipwa na mteja na inatoa fursa ya kupata tenda kwa kampuni.

Akizungumza katika mahojiano maalum na HabariLeo, Ofisa Huduma Elimu kwa Mlipa Kodi TRA Ofisi za Geita, Justine Katiti, amesema VAT haiongezi gharama ya kodi bali inalipwa kwa thamani ya faida ya utoaji huduma kwa mteja.

“Niwaondoe hofu wafanyabaishara kwamba ukisajiliwa kwenye VAT kwamba kunaongeza gharama (ya kodi) hamna gharama yeyote, sana sana inampa nafasi mfanyabiashara atakapoenda kununua bidhaa mfano pikipiki atakapokwenda kununua pikipiki atalipa VAT kule.

“Atakapokuja kuuza ile pikipiki atajirejeshea kwanza ile VAT aliyolipa kule alipokwenda kununua ule mzigo, kwa hiyo ni faida kwamba, unapokuwa umesajiliwa kwenye VAT unapouza ile bidhaa unajirejeshea kwanza ile gharama ya VAT” amefafanua.

Katiti amewataka wafanyabiashara kuendelea kufanya biashara kwa miongozo, ili kuunga mkono juhudi za serikali kuboresha huduma za kijamii kwa kuwa kodi inayotozwa inarejea moja kwa moja kwenye huduma za kijamii.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/bd7bdf56a23cdef58c635146b320328b.jpg

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mradi wa ...

foto
Mwandishi: Yohana Shida, Geita

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi