loader
RUWASA yafanya kweli maji Mpanda

RUWASA yafanya kweli maji Mpanda

ZAIDI Sh bilioni 1 zimetumika kujenga miradi miwili ya maji katika kata mbili za Uruila na Kapalala, zilizopo Halmashauri ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda, mkoani Katavi.

Miradi hiyo inatekezwa na Mamlaka ya Usambazaji wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).

Akizungumza na Daily News Digital, Mhandisi Mkuu RUWASA Wilaya ya Mpanda, Elinathan Karagwe, amesema katika mradi mkubwa wa maji uliopo Kijiji cha Mtakuja kata ya Kapalala, walipokea kiasi cha Sh milioni 600 kutoka Mfuko Mkuu wa Maji.

"Mradi unaendelea kutoa huduma ya maji kwa wakazi wapatao 7,200 katika vijiji viwili vya Mtakuja na Songambele, mradi huu umeleta manufaa makubwa sana kwa wananchi wa vijiji hivi, kwa sababu walitumia maji yasiyo salama, " amesema Karagwe na kuongeza kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka 2018 ulikamilika Desemba 2021.

Ameongeza kuwa walipokea kiasi cha Sh milioni 450 fedha zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan,  zilizotokana na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 kwa ajili ya  ujenzi wa mradi wa Kijiji cha Ikondamoyo Kata ya Uruila ambao ulianza Februari na unatarajia kukamilika mwishoni mwa Juni mwaka huu.

"Mradi huu ukikamilika tunatarajia kuwahudumia zaidi ya wananchi 2500 na tutajenga vituo 6 vya maji, ambapo tutaweka katika shule ya msingi Ikondamoyo katika Kituo cha Afya na maeneo mengine," amesema.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikondamoyo, Philipo Mswanya amepokea kwa furaha mradi huo wa maji, ambapo amesema kwa sasa wananchi hufuata maji umbali mrefu na hupokea kesi nyingi zinazohusu migogoro ya wanandoa kuchelewa kurudi nyumbani kwa ajili ya kufuata maji.

foto
Mwandishi: Swaum Katambo, Katavi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi