loader
Tiketi VIP A Yanga v Simba zimeuzwa

Tiketi VIP A Yanga v Simba zimeuzwa

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limesema tiketi za VIP A kwa mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kati ya Yanga na Simba zimeuzwa.

Mchezo huo unatarajiwa kufanyika Jumamosi Mei 28, 2022 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa ya TFF iliyotolewa leo Alhamisi, Mei 26,2022, imeeleza kuwa tiketi zote za VIP A zimeuzwa, ambapo kiingilio ni Sh 30,000, ingawa haikusemwa ni tiketi ngapi za VIP A. Viingilio vingine kwa mchezo huo ni Sh. 10,000 eneo la mzunguko, ambalo kwa kawaida ndiyo hukaa mashabiki wengi na Sh. 20,000 kwa VIP B.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/512196fb97be4de6edbd6788270ec96d.jpg

RAIS Samia Suluhu Hassan, amewapongeza wachezaji ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi