TAASISI ya Mama Ongea na Mwanao, imemteua muigizaji wa filamu nchini, Yvonne Cherry maarufu Monalisa, kuwa Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo.
Monalisa ameweka wazi mapema leo Mei 26, 2022, kwenye mtandao wake, akishukuru kwa nafasi hiyo aliyoteuliwa na kuahidi kuifanyia kazi katika kutimiza malengo.
"Ninaishukuru Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao kwa kunichagua kuwa Katibu Mtendaji wa Taasisi hii. Nami naahidi, kuifanya kazi yangu kwa weledi mkubwa na kuhakikisha taasisi inatimiza malengo yake iliyojiwekea.
"Pia naahidi kusimamia na kuchochea taasisi kufanya miradi mingi zaidi ya kijamii kwa kushirikiana na wajumbe, jamii husika na wadau mbalimbali wa maendeleo.
"Kwa taasisi ya Mama ongea na mwanao kazi ndio inaanza rasmi," ameandika Monalisa.