loader
UVCCM Nyamagana wampongeza Rais Samia

UVCCM Nyamagana wampongeza Rais Samia

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi mbalimbali katika kuwaletea maendeleo Watanzania.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Nyamagana, Boniphace Zephania, wakati wa utoaji wa tamko la kumpongeza Rais Samia.

Amempongeza Rais Samia kwa kusikia kilio cha wafanyakazi na kuwaboresha maslahi yao.

Naye Mwenyekiti kundi la mabalozi wa kujitolea wa Sensa Tanzania,Mansuli Jumanne,  amewaomba vijana kuweza kuhamasisha jamii ishiriki ipasavyo katika sensa.

Pia amempongeza Rais Samia kwa kuwa miongoni mwa viongozi 100 bora duniani na pia kwa kuruhusu uhuru wa vyomba vya habari nchini.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/13e3668f413fcfa927b5c844f8c3b308.jpg

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mradi wa ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi