TAMASHA la muziki wa dansi la Wafia Dansi litakalowahusisha waimbaji wa mikoani kufanyika Mei 28, 2022 ukumbi waTCC Club Gwambina, Dar es Salaam.
Tamasha hilo lililoandaliwa na Cheza Kidansi Entertainment na Patrick Kessy 'Kilimo Kwanza', ni miongoni mwa matamasha makubwa duniani.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam, Mratibu wa tamasha hilo, Bernard James, amesema kuwa tamasha hilo litasindikizwa na Mapacha, Walugulu na Mjengoni Classic.
"Tamasha la Wafiadansi linalokutanisha wanamuziki wa dansi na wadau wake na watu wengine kutoka nchi mbalimbali mashabiki kushuhudia burudani italeta umoja na mshikamano kwa wanamuziki na kuleta tija kwa tasnia ya muziki wa dansi hata kukuza muziki wa dansi Tanzania," amesema.