loader
Serikali yawaahidi raha Mvumi

Serikali yawaahidi raha Mvumi

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, David Silinde amesema, serikali inaendelea kutafuta rasilimali, ili barabara ya mvumi Wilayani Chamwino mkoani Dodoma ijengwe kwa kiwango kwa lami.

Silinde ameyasema hayo leo  Mei 26, 2022 wakati wa ziara yake ya kukagua barabara iliyojengwa kwa kiwango cha lami kilometa 1 kuanzia eneo la makaburini hadi Bilia kata ya Mvumi Mission Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.

Wakati wa ziara hiyo Mbunge wa Jimbo la Mvumi, Livingstone Lusinde aliwasilisha ombi la wananchi wake kutaka kuongezewa barabara ya lami, ili kuongeza hadhi ya kata hiyo na kurahisisha shughuli za usafirishaji.

Silinde amesema suala hilo litafanyiwa kazi na atahakikisha anasimamia utekelezaji kwa vitendo ili barabara hiyo ipate lami ya kutosha kuipa hadhi Mvumi kuwa mji mdogo.

“Tuendelee kumuombea Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kumuunga mkono, ili aweze kufanya mambo makubwa zaidi kama mnavyoona kwenye utekelezaji wa miradi na sisi wasimamizi wake tutaendelea kuisimamia kwa vitendo, niwahakikishie Mvumi mtaongezewa lami zaidi ya Kilomita 2, ” amesema Silinde.

Amesema ameridhishwa na ukaguzi aliofanya katika barabara hiyo, kwa kuwa asilimia kubwa umekamilika na amemuelekeza Meneja Wakala wa Barabara za Mjini na Vjijini (TARURA) kuandaa bajeti ya uwekaji wa taa za kwenye barabara hiyo .

Naye Mbunge wa Jimbo la Mvumi, Livingstone Lusinde, amemshukuru Rais Samia kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuhakikisha wanaisimamia TARURA kwa kutekeleza miradi ya ujenzi wa barabara  na ameishukuru  Serikali kuridhia ombi la wananchi kuongezewa kilomita za lami.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/841cb6d7743e4090bc39dcd64084b672.jpg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi