Klabu ya soka ya Chelsea imefikia muafaka wa mauzo na muungano unaoongozwa na mfanyabiashara Mmarekani Todd Boehly, baada ya mmiliki wa Urusi na bilionea Roman Abramovich kuwekewa vikwazo na serikali ya Uingereza.
Makubaliano ya "mwisho na ya uhakika" yalifikiwa mwishoni mwa Ijumaa, klabu hiyo ilisema katika taarifa, na shughuli hiyo ikitarajiwa kukamilika Jumatatu.
Bodi ya kitengo kikuu cha soka nchini Uingereza, Premier League, iliunga mkono mauzo ya Chelsea kwa mmiliki mwenza wa Los Angeles Dodgers Todd Boehly na wanachama wa Clearlake Consortium kwa karibu dola bilioni 5.3 mapema wiki hii.