loader
Papa francis kuzuru ukraine … lakini

Papa francis kuzuru ukraine … lakini

Papa Francis amesema anatarajia kuzuru Ukraine lakini anasubiri "wakati mwafaka wa kufanya hivyo," amesema katika hafla ya watoto iliyofanyika Vatikani.

Mtoto mkimbizi wa Ukrainia aitwaye Sachar alimwomba papa kama angeweza kuja Ukrainia "kuwaokoa watoto wote wanaoteseka huko sasa."

Francis alimjibu Sachar kwamba "Nafikiri sana kuhusu watoto nchini Ukrainia." Papa alisema kwamba “angependa kwenda Ukraine. Lakini, inabidi ningojee wakati mwafaka wa kuifanya hivyo, kwa sababu si rahisi kufanya uamuzi ambao unaweza kuleta madhara zaidi kwa ulimwengu wote kuliko wema. Ni lazima nitafute muda mwafaka wa kufanya hivyo.”

Francis aliongeza kuwa atakutana wiki hii na maafisa wa Ukraine ili kujadili ziara inayowezekana.

Ametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano lakini amepokea ukosoaji kutokana na kukataa kumlaani Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kuanzisha uvamizi huo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/609cdaf5cdd849a8abe225920592d3cd.jpeg

RAIS Mstaafu wa Awamu ya ...

foto
Mwandishi: KYIV, Ukraine

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi