loader
Mayele, Feisal wachomoza bungeni

Mayele, Feisal wachomoza bungeni

WACHEZAJI wa Yanga, Fiston Mayele na Feisal Salum leo wametajwa bungeni wakati Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, akiwasilisha makadiri ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2022/23 bungeni mjini Dodoma.

“Naomba nitumie nafasi hii kumuomba radhi bosi wangu, Waziri Mkuu kwa kitendo alichokifanya Fei Toto (Feisal Salum) kule Mwanza. Bosi niwie radhi nilivyompeleka Fei Toto Yanga sikujua atakuja kuwafanyia kitu mbaya namna hii.

“Nasikia anatafutwa na maliasili eti kaua mnyama bila kibali. Nakupongeza Anthony Mavunde wewe ndiye ulikuwa Mwenyekiti wa kusaidia Yanga ikiwa kwenye mapito,” amesema Waziri Nchemba na kupongeza usajili wa Fiston Mayele ambaye amesema amekuwa maarufu sana.

Pia Waziri Nchemba aliipongeza timu ya Simba kwa kwa kuwakilisha vyema kwenye mashindano ya kimataifa.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/22f0d7a3cc99bfc7143305c5252c49d6.jpg

ZAIDI ya Vijana 25,000 kutoka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi