loader
Maandalizi sensa yafikia asilimia 87

Maandalizi sensa yafikia asilimia 87

WAZRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema maandalizi ya sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agosti 23, 2022 imefikia asilimia 87.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo bungeni mjini Dodoma kwenye hotuba yake ya kuahirisha mkutano wa saba wa Bunge la 12.

Kwa upande mwingine nitumie fursa hii kuliarifu Bunge lako tukufu kuwa maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, yanaendelea vizuri na yamefikia asilimia 87.

“Niwaombe waheshimiwa wabunge wenzangu hususan wanaporejea kwenye maeneo yao ya uwakilishi kuendelea kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye zoezi hilo muhimu.

“Vilevile, nitoe wito kwa Watanzania wote kujiandaa kuhesabiwa ikiwa ni pamoja na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa makarani wa sensa na viongozi wetu kwenye maeneo tunayoishi,” amesema Waziri Mkuu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/412362936f53148c7e7bcfd000109b06.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi