loader
Majaliwa azipongeza Simba, Yanga kutangaza utalii

Majaliwa azipongeza Simba, Yanga kutangaza utalii

WAZRI Mkuu Kassim Majaliwa, amezipongeza klabu za Simba na Yanga za Dar es Salaam kwa kutangaza utalii wa Tanzania.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo bungeni mjini Dodoma kwenye hotuba yake ya kuahirisha mkutano wa saba wa Bunge la 12.

“Mwisho kwa upande wa michezo niwapongeze sana Dar Young Africans (Wananchi) kwa kuibuka vinara wa Ligi Kuu ya NBC kwa msimu wa 2021/2022.

“Hongereni sana wananchi, mmekuwa na msimu mzuri sana na mmestahili kuibuka mabingwa.

Mheshimiwa Spika, miongoni mwa matukio yaliyonivutia wakati wa shamrashamra za ubingwa wa wananchi ni kitendo chao cha kukumbuka kuitangaza Tanzania kupitia Royal Tour na kuhamasisha ushiriki wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, kama ambavyo klabu ya soka ya Simba ilivyoanzilisha kuitangaza tanzania kwenye medani za soka za kimataifa kupitia jezi zao kuandikwa Visit Tanzania.

“Niendelee kutoa wito kwa vilabu na makundi ya Watanzania wanaosafiri nje kuhakikisha wanatumia jezi zetu zenye kubeba jumbe au ajenda za kitaifa kwani jukumu la kuitangaza Tanzania na ajenda zake za kitaifa ni letu sote,” amesema.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f84ddf4f4f4f6a799bca6ba498b583dd.jpg

SIMBA Queens imekuwa timu ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi