loader
CRDB yatoa gawio la bilioni 36.1/- serikalini

CRDB yatoa gawio la bilioni 36.1/- serikalini

Benki ya CRDB imetoa gawio la Sh bilioni 36.1 serikalini katika hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk Ally Laay, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela walimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba hundi ya kiwango hicho cha fedha Jumatano (Juni 29, 2022).

Mbali na Waziri wa Fedha, wengine waliohudhuria tukio hilo ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais - Tamisemi, David Silinde, Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Patrobas Katambi pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence M

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Fedha aliipongeza Benki hiyo kwa kutoa gawio kwa Serikali, Dk Nchemba aliipongeza Benki ya CRDB kwa kupata matokeo mazuri ya fedha mwaka 2021 ambayo yamechangia ongezeko la gawio kwa wanahisa ikiwamo Serikali.

Dk Nchemba alisema fedha zilizopatikana kupitia gawio hilo zitakwenda kusaidia utekelezaji wa miradi ambayo Serikali imeianisha katika vipaumbele vya Bajeti ya mwaka 2022/2023.

Aliipongeza Benki ya CRDB kwa matokeo mazuri ya fedha iliyopata katika nusu ya kwanza ya mwaka huu 2020 ambapo faida ya Benki imeongezeka kwa asilimia 111 kufikia Shilingi bilioni 90 kutoka Shilingi bilioni 43 zilizoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2021.

“Mkiendelea na kasi hii mwakani tunategemea kupata gawio nono zaidi…Kipekee kabisa niipongeze Bodi, Menejimenti na wafanyakazi wote wa Benki ya CRDB kwa kazi nzuri mnayoifanya,” Waziri Nchemba alieleza.

Alizitaka Taasisi na Mashirika yote ambayo Serikali inahisa kuweka mikakati madhubuti itakayoleta tija, huku akiwataka viongozi wake kujitathmini kiutendaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema kuwa gawio hilo ni sehemu ya faida ya Shilingi bilioni 268.2 baada ya kodi ambayo Benki hiyo imeipata katika mwaka wa fedha 2021.

Pia ameeleza kuwa Benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora ili kukidhi mahitaji ya wanahisa wake na wananchi kwa ujumla.

 

 

 

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f7a67b7b71d447065fde99405ac952e8.jpg

UKOSEFU wa elimu ya biashara, uthubutu na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi