loader
Mradi ufuatiliaji wahitimu DIT watoa mwanga

Mradi ufuatiliaji wahitimu DIT watoa mwanga

MATOKEO ya mradi wa ufuatiliaji wahitimu (Tracer Study) wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), imeonesha kuwa asilimia 69 ya wahitimu wanaajirika na kujiajiri, huku asilimia asilimia 31 pekee ndio hawajaajirika.

Hayo yamesemwa leo na Mhadhiri wa DIT,   Dk. Ambele Mtafya katika uzinduzi wa ripoti ya awali ya mradi unaolenga kutambua ufanisi wa mitaala ya taasisi pamoja na hali ya soko kwa wahitimu wake.

Dk. Mtafya ambaye pia ni  Mwenyekiti wa mradi huo, amesema kwa mwaka 2020 wanawake walioajiriwa ni asilimia 1.9, ambao wapo kwenye mafunzo ya vitendo asilimia 2.9, ambao wameendelea na mafunzo kwa ngazi nyingine ya elimu ni asilimia 1.9 na ambao wamejiajiri ni asilimia 1.4, huku ambao hawana ajira ni asilimia 4.8.

Amesema kwa upande wa wavulana ambao wapo kwenye ajira ni asilimia 22.6, ambao wameendelea kwa ngazi nyingine ya mafunzo ni asilimia 14.4, ambao wapo kwenye mafunzo ya vitendo ni asilimia 7.2, waliojiajiri ni asilimia 13.5 na wanaofanya kazi kwa kujitolea ni asilimia 4.3, hivyo kufanya idadi ya asilimia 31.7 ya  wahitimu wa DIT kwa mwaka 2020 kutoajiriwa.

Amesema lengo la tathmini hiyo ni kuangalia baada  ya kumaliza shule, changamoto gani wamekumbana nazo wahitimu katika soko la ajira.

“Tunafanya hivi kwa sababu unapoenda hospitali daktari atakupima kutafuta viashiria vya ugonjwa, hivyo na sisi bidhaa zenu ni wanafunzi, walaji ni waajiri tujue wanakubalika au la, ili tujue kama bidhaa haikubaliki labda mtaala wetu unashida au ni wao wamekosa umahiri” amesema Dk. Mtafya.

 Amesema takwimu zinaonesha kuwa asilimia ya wanawake katika soko ni wachache kuliko wanaume, katika takwimu pia zimeonesha ambao hawajaingia soko la ajira ni asilimia 31.

“Changamoto wakati mwingine sio umahiri ila wakati mwingine tatizo la kujiajiri ni kukosa mitaji, hivyo tunaomba serikali na wadau kuboresha elimu za ujasiriamali, lengo letu kubwa mwanafunzi akimaliza DIT awe anatafutwa,” amesema.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c282058897851d6ae127cc1644d8d047.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi