loader
Kiwanda cha kuchakata taka chazinduliwa Dar

Kiwanda cha kuchakata taka chazinduliwa Dar

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Amos Makalla amezindua kiwanda cha kuchakata taka na kuzigeuza kuwa mbolea halisi cha Mabwepande kilichojengwa kwa gharama ya Sh Bilioni 6.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Makalla amesema kiwanda hicho kimekuja wakati muafaka, ambao bei ya mbolea imepanda kutokana na vita inayoendelea baina ya Urusi na Ukraine na kutoa wito kwa wananchi kununua mbolea hiyo.

Kiwanda hicho ni ufadhili wa Serikali ya Ujerumani na Tanzania kupitia ushirikiano baina ya Jiji la Dar es salaam na Jiji la Hamburg.

Amesema uwezo wa Mkoa huo ni kuzalisha zaidi ya tani 23 za taka kwa siku, hivyo kupatikana kwa kiwanda hicho itasaidia kuwa na uhakika wa mahala pa kuzipeleka.

Makalla ametoa wito kwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kusimamia vizuri uendeshaji wa kiwanda kuhakikisha uzalishaji wa malighafi unakuwa wa kutosha.

Pamoja na hayo Makalla amesema kuwa siku ya kesho, Meya wa Jiji la Hamburg na Meya wa Jiji la Dar es salaam wanatarajia kusaini mkataba wa ushirikiano katika kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/08fa626cfef47c12fca121bcb8dbd0d6.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Brighiter Masaki

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi