loader
Kitabu cha Kwaheri kuzinduliwa Dar J’pili

Kitabu cha Kwaheri kuzinduliwa Dar J’pili

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, Julai 3 mwaka huu, anatarajiwa kuziongoza taasisi kadhaa zinazohusiana na Kiswahili nchini katika uzinduzi wa kitabu cha Kwaheri.

 Uzinduzi wa kitabu hicho kilichopo katika mfumo wa riwaya unatarajiwa kufabnyika ukumbi wa NSSSF Mafao House, Dar es Salaam.

Siku hiyo ya uzinduzi ni maalumu ya mjue mtunzi iliyoandaliwa na Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira (UWARIDI), ikishirikiana na Mdhamini Mkuu, Elite Bookstore.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, mwandishi wa kitabu cha Kwaheri, Hassan Ally Hassan, alisema taasisi kadhaa zitashriki.

Aliztaja kuwa ni Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA), Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI), Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania, Taasisi inayohusiana na masuala ya hatimiliki (COSOTA) na wizara mbalimbali.

Pia amesema kutakuwa na wahadhiri mbalimbali wa vyuo vikuu, wasomaji na wapenzi wa kazi za fasisi na wadau wengine mbalimbali wa Kiswahili.

Alisema lengo la kuandika kitabu cha Kwaheri ni kuleta mabadiliko ya kifikra katika jamii, hasa kwa wanafunzi  wa shule za sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu, wanaosoma fasihi kwa kuja na riwaya ya usasa ambayo inawawezesha wasomaji kupata maarifa halisi kupita kazi ya fasihi.

“Riwaya hii inaelezea mapito ya kiutawala na masuala ya kijamii yanayoibuka na kuleta tafakuri kwa wana jamii kuhusiana na utamaduni, matakwa ya vijana yanayogongana na yale ya wazee na matarajio ya jamii; Suala la utaifa na matatizo yake.

“Pia kimesheheni masuala ya elimu, sayansi, siasa, utalii, tiba, uzalendo, umaskini, magonjwa, mapenzi na ndoa, rushwa, uongozi mbaya, umuhimu wa elimu pamoja na ufujaji wa mali za umma,” alisema.

Amesema ameandika kitabu hicho, ili kutoa mchango wake wa kuusaidia mfumo wa elimu Tanzania.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/4a6d32a4cb90a18b529fd3e12276ebbb.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi