loader
Vyuo vyapewa changamoto tasnia ya habari

Vyuo vyapewa changamoto tasnia ya habari

WIZARA ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, imevitaka vyuo na taasisi zinazotoa taaluma ya uandishi wa habari kufanya tathimini ya mchango wao katika kukuza na kuendeleza tasnia ya habari.

 

Amesema tathmini hiyo ambayo inapaswa kuhusisha wadau wa habari itasaidia kujua mahitaji ya wanataaluma wanaohitajika kwenye soko na sio kufanya kiholela, kila mtu kujiona anafaa kwenye kazi hiyo.

 

Hayao yamesemwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, wakati akifungua kongamano la maadhimisho ya miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, lililolenga kuangalia mchango wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC).

 

Amesema tathmini na makongamano hayo yatasaidia kuona uhitaji uliopo mtaani na kufanya mabadiliko ya mitaala kulingana na uhitaji wa wanataaluma waliopo na kuweka uthamani wa kazi wanazofanya.

 

“Hili ni jambo kubwa linalojenga utamaduni wa kufanya tathmini na kuchambua mapungufu yaliyopo katika mfumo wa kuwaandaa wanahabari.

 

“Majukumu yetu kama wanahabari ni kupasha habari, kuelimisha na kuburudisha jamii kwa weledi wa hali ya juu. Pamoja na kupeleka habari katika jamii, wanahabari tunapaswa kuwa sauti ya wananchi, na wao kuona umuhimu wa kazi tunazozifanya na sio kuona ni kazi rahisi inayoweza kufanywa na mtu yoyote,” amesema.

 

Nape amesema serikali inafanya juhudi kubwa kufungua fursa mbalimbali zinazolenga kuboresha tasnia ya habari, lakini bado kuna changamoto nyingi zinazoikabili sekta hiyo.

Miongoni mwa changamoto hizo ni bado tasnia ya habari kutokuwa na hadhi inayostahili hali inayosabashaisha wasio wanataaluma kuvamia, inatakiwa kuwe na hadhi ya kutofautisha wenye taaluma na wasio na taaluma.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7998268b4b9fbea4e1a8559c09ddd1e4.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Brighiter Masaki

1 Comments

  • avatar
    Rommel Mauma
    01/07/2022

    Mgumo wa habari unabadilika kutoka wa gazeti na redio kwenda kidijitali. Tulizoea kupata maudhui ya habari gazetini au redioni zilizohaririwa kuhakikisha lugha sanifu na ukweli [verification]. Tulikaa na kuegemea vitini kusoma na/au kusikiliza taarifa za habari kwa saa maalumu zilizotengwa upatikanaji wa gazeti na/au usomaji wa tssrifa ya habari. Mfumo ulikuwa unatuletea habari, kama tukio [event]. Vyombo vya habari wengine wakaviita, *,Mhimili wa Nne - Fourth Estate* na/au *Walinzi wa Lango - Gatekeepers*. Kuta za jengo zina nyufa shauri ya habari za mitandao ya jamii [blogs, viblogs Mfumo wa dijitali unaovuma [trending and streaming] unatutaka tukae na kuinamia mbele [hasa mfumo wa "online blogs and vlogs" kwa simu za viganjani]. Habari za mitandao ya jamii mingi sana hazitoi habari, kulingana na taaluma ya uandishi wa habari. Habari za *print/photos* hubandikwa, *kikanjanja-kanjanja*. Wapo wanaoamini kuwa aina hiyo haiwezi kuitwa ya uandishi wa habari; japo imebandikwa jina la *community journalism*. Haina tofauti na uandishi wa barua binafi *personal letter*, ambayo haina m/wahariri. Zaidi, ni vigumu kuihakiki *[verifiable]*.

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi