loader
Wanafunzi Chuo cha Kenya wajivunia ujuzi DIT

Wanafunzi Chuo cha Kenya wajivunia ujuzi DIT

WAHITIMU 33 wa chuo cha Kisumu National Polytechinic cha nchini Kenya, wamehitimisha mafunzo ya siku 21 ya kubadilishana ujuzi katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, Kampasi ya Mwanza.

Pamoja na mambo mengine, wamejivunia kupata ujuzi wa kutengeneza viatu vya ngozi vilivyofunikwa na vya wazi, masomo ambayo hajatolewi chuoni kwao.

“Na kila mmoja ameweza kutengeneza jozi moja moja ya viatu vya kufunikwa na vya wazi. Hii ni kwa sababu tumepata muda wa ziada wa kufanya mazoezi zaidi kutokana na kuwa na walimu wazoefu hapa DIT,” amesema kiongozi na mwalimu wa wanafunzi hao, Mariam Cassim, ambaye naye alikuwa akijifunza.

Amesema chuoni kwao mafunzo ni ya kushona mavazi tu, hivyo, wanaenda kueneza elimu na ujuzi waliopata Tanzania.

Mafunzo ya kubadilishana ujuzi ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Kujenga Ujuzi kwa Maendeleo na Uingiliano wa Kikanda katika Afrika Mashariki (EASTRIP), unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa gharama ya Sh 37 billioni.

Unatekelezwa kuanzia mwaka 2019 nchini Tanzania, Kenya na Ethiopia, ambapo wanafunzi na walimu wamekua wakitembeleana kubadilisha ujuzi.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/cb8b737734503947c0e7aa927ecd2128.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Abela Msikula, Mwanza

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi