loader
Wanafunzi Dar waelimishwa matumizi ya mitandao

Wanafunzi Dar waelimishwa matumizi ya mitandao

WANAFUNZI wa Shule za Sekondari za Benjamin Mkapa na St. Anne Marie zilizopo jijini Dar es Salaam, wamepewa elimu juu ya fursa za mitandaoni na mbinu salama za matumizi ya mitandao katika kuadhimisha Siku ya Mitandao ya Kijamii, ambayo huadhimishwa Juni 30 kila mwaka.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Success Hands Initiative, Marynisa Mangu alisema: “Tumejizatiti kuhakikisha jamii inachangamkia fursa za kidigitali, huku ikiendelea kuwa salama katika matumizi ya kimtandao.

“Tumekuwa tukishirikiana na shule ya Benjamini Mkapa, St.Anne Marie na shule nyingine, ili kuwaandaa vijana ambao wataanza kutumia mitandao ya kijamii kwa faida zaidi na siyo kutumia mitandao ya kijamii katika mambo yasiyofaa,” alisema Mangu.

Naye mwanzilishi wa Natokaje Kidigitali, Getrude Mligo aliwataka wanafunzi hao kuwa wabunifu na kutumia ubunifu wao kutafuta namna ya kuuza ubunifu huo kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Getrude alinukuliwa akisema: “Kuna stadi nyingi za kujifunza ambazo zinaweza kukufanya ujiajiri au kuajiriwa. Tujifunze kusoma kozi fupi za mitandaoni, zipo kozi nyingi kwenye majukwaa kama Coursera, Udemy, Future Learn, Google Garage na zinatolewa bure kabisa, hizo fursa zote tusiziache zipite, tuzichangamkie wadogo zangu,” Getrude aliwaambia wanafunzi.

Akieleza juu ya mafanikio ya kampeni hiyo itakayohitimishwa na mkutano wa wadau utakaofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Jumamosi Julai 2, 2022 alisema:

“Mpaka sasa tumewafikia wanafunzi takribani 440 katika shule mbili, na kati yao tumepata mabalozi zaidi ya 26 ambao wataendelea kupata mafunzo kwa miezi 6 zaidi na baadae mabalozi hao wanategemewa kufikisha elimu hiyo kwa wenzao wengine 2300,” alibainisha Getrude.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/05bb3248f0b3df5a151085212257bae5.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi