loader
Dk Mwinyi kumwakilisha Samia Burundi

Dk Mwinyi kumwakilisha Samia Burundi

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amekwenda Jamhuri ya Burundi kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika sherehe za miaka 60 ya uhuru wa nchi hiyo zinazotarajiwa kufanyika leo.

Taarifa kwa vyombo vya habari jana ilieleza kuwa katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume, Dk Mwinyi aliagwa na viongozi wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah.

Katika safari hiyo, Dk Mwinyi amefuatana na viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo mkewe, Mama Mariam Mwinyi.

Burundi ilipata uhuru Julai Mosi mwaka 1962 kutoka kwa Ubelgiji ikiongozwa na Mwami Mwambutsa.

Nchi hiyo ilijiunga na Umoja wa Mataifa (UN) Septemba 1962 na ikawa Jamhuri mwaka 1966 chini ya Rais Michel Micombero.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d79c6f6e5e62942bd7a68a89e4a9cb24.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi