loader
Geita wapokea Sh Bil 416 miradi ya kimkakati

Geita wapokea Sh Bil 416 miradi ya kimkakati

MKOA wa Geita umepokea jumla ya Sh. bilioni 416 ndani ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati inayotarajiwa  kuibua mapinduzi ya kiuchumi mkoani hapa.

Hayo yamelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule katika hafla ya kumpongeza na kumushukuru Rais Samia suluhu kwa miradi ya maendeleo anayoendelea kuitekeleza mkoani Geita.

Senyamule ametaja baadhi ya miradi ya kimkakati ni ujenzi wa stendi ya mabasi ya wilaya ya Chato-Kahumo iliyogharimu jumla ya Sh. bilioni 12.3, ambazo zote zimetumika na utekelezaji upo katika hatua za ukamilishaji.

“Pia kuna ujenzi wa soko la kisasa katika mji mdogo wa Katoro katika halmashauri ya wilaya ya Geita, uliogharimu Sh. bilioni 1.8 ziliizotolewa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) kupitia mfuko wa uwajibikaji wa makampuni kwa jamii (CSR).

“Pia kuna mradi wa ujenzi wa kiwanda cha asali katika halmashauri ya Bukombe, ambapo fedha zilizopokelewa ni Sh. Milioni 504, zimetumika zote na ujenzi umekamilika, mitambo imeshafungwa na kiwanda kimeshanza kuzalisha asali.”

Ameeleza pia kuna ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu unaotarajiwa kugharimu Sh bilioni 2.4, na hadi sasa tayari Sh bilioni 1.3 zimeshatumika, huku ujenzi wa hospitali ya rufaa ya kanda Chato na hadi sasa jumla ya Sh. bilioni 34 zimeshapokelewa.

Senyamule amesema, mradi wa uwanja ndege Chato umetumia jumla ya Sh. bilioni 45, huku mkoa umeshapokea kiasi cha Sh. bilioni 4.8 kwa ajili ya ujenzi wa soko la kisasa la mifugo na mradi umeshakamilika.

Ameongeza, pia mwaka huu mkoa umepokea Sh. bilioni 13.9 kwa ajili ya mradi wa kilimo cha umwagiliaji, Sh. bilioni 25 kwa ajili ya usambazaji umeme katika vijiji 144, pamoja na Sh. bilioni 13 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wazazi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/298bfaf7eea5b3a84bc96df6122e5182.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Yohana Shida, Geita

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi