loader
Geita raha mradi mkubwa umwagiliaji

Geita raha mradi mkubwa umwagiliaji

SERIKALI imetenga kiasi cha Sh bilioni 13.9 kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa kilimo cha umwagiliaji katika mkoa wa Geita, ambao utatekelezwa kwenye halmashauri tatu mkoani hapa.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule, wakati akizungumuza na watumishi wa umma katika hafla ya mkoa kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa miradi ya maendeleo.

Senyamule amesema Geita ni miongoni mwa mikoa ambayo imeingiza kwenye awamu ya kwanza ya mradi wa kilimo cha umwagiliaji na utatekelezwa katika halmashauri za Nyang’hwale, Geita Mji na Chato.

“Hayo ni mambo makubwa anayoyafanya mheshimiwa Rais, kama tulikuwa tunalima mpunga kwa kutegemea mvua, mara moja kwa mwaka, tutaenda kulima mara mbili, na tukivuna tunalima tena kwa sababu maji ya kumwagilia yapo.

“Kwa hiyo sisi tumebahatika, tumetengewa kwa Nyang’hwale Sh. bilioni nne, mradi wa Ibanda ambayo ni Geita Mji ni Sh. bilioni 6.5 na halmashauri ya Chato ni Sh. bilioni 3.4, kwa hiyo Geita tuna miradi mikubwa mitatu ya umwagiliaji ambayo itatekelezwa,” ameeleza.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Zahra Michuzi amesema tayari wameshatenga eneo kwa ajili ya mradi huo ambao utaongeza fursa za kiuchumi, uhakika wa chakula pamoja na ajira.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/185736513b065a458821ea763a335918.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Yohana Shida, Geita

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi