loader
TLS yasema dawa ya mawakili vishoka imepatikana

TLS yasema dawa ya mawakili vishoka imepatikana

CHAMA cha Wanasheria  nchini (TLS), kimesema mihuri mipya ya kielekroniki itasaidia kudhibiti vishoka, ambao wamekuwa na tabia ya kutumia mihuri hiyo bila idhini ya wahusika.

Akitoa Taarifa  hiyo leo, Rais wa TLS Prof. Edward  Hoseah  amesema wamekuwa  wakipokea malalamiko ya mihuri kutumiwa na vishoka na wengine  kupatikana ikitumika ‘stationeries’ huku wakiripoti kupotea.

Ameeleza kuwa mihuri hiyo ya kieletroniki itazuia tatizo la vishoka wa uwakili wanaotumia mihuri ya mawakili kiholela kinyume na taratibu.

“Mwezi Mei 26 mwaka 2022, TLS ilifanya uzinduzi wa mihuri ya kieletroniki kwa mawakili wa Tanzania katika Mkutano huo muongozo wa matumizi ya mihuri hiyo ulioneshwa na tumetoa ufafanuzi huo,” amesema.

PAmesema tayari kuna mamlaka mbalimbali ambazo zilianza kukataa mihuri ya mawakili kwa sababu ya uwepo wa mihuri feki, au kutumika kwa mihuri na mawakili feki au mihuri ya mawakili halali kutumika bila ruhusa yao.

 Hivyo alisema mihuri hiyo inarudisha imani kwa uma na kukubaliwa kwa mihuri ya mawakili, kwa kuwa haitaweza kutumika hovyo.

“Mihuri hii ina namba ya siri  ambayo itakuwa inafahamika na kutumiwa na wakili husika tu na haitakuwa rahisi kutumika na mtu mwingine. Pia mihuri hii itakuwa na QR Code itakayowezesha kufanya uhakiki wa usahihi wa muhuri,”alibainisha.

Ameeleza kuwa  Mmhuri hiyo itatumika kwa mawakili wote kwa taratibu na sheria zilizopo au zitakazowekwa, kwani  hakuna sheria iliyobadilishwa.

Amesema mihuri haitakuwa inahuishwa kila mwaka isipokuwa leseni ya uwaklli.

Prof. Hosea amesema lengo la mihuri hiyo ni kuilinda tasnia ya sheria dhidi ya matendo mabaya, hivyo Mawakili hawabebeshwi mzigo wa gharama, bali itadhibiti kupoteza kipato ambacho kingepaswa kupokelewa na wakili, husika kwani kinapokelewa na kishoka.

“Mihuri hii inatumia mfumo maalum hivyo, kwa wakili ambaye atakuwa hajahuisha leseni yake katika muda anaotakiwa kuhuhisha leseni yake, hataweza kutumia muhuri wake hadi atakapohuisha leseni yake.

 ”Kila muhuri una namba maalum, hivyo wakili akitoa taarifa kuwa muhuri wake umepotea hatua ya kwanza kabla hajapewa muhuri mwingine itakuwa ni kuuzuia/kuusitisha muhuri,” amesema.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d465ad356822d5da566380b521d4b7d2.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Aveline Kitomary

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi