loader
Dar, Hamburg wasaini makubaliano sekta 5

Dar, Hamburg wasaini makubaliano sekta 5

JIJI la Dar es Salaam limesaini hati ya makubalino na Jiji la Hamburg lililopo Ujerumani katika sekta tano ikiwa ni kuimarisha ushirikiano wa majiji hayo ambao umedumu kwa miaka 12.

Hati zilizosaini leo katika ukumbi wa Karimjee ni kushirikiana katika sekta ya Afya, Elimu, Ujasiriamali, Utamaduni na kupendezesha mji wa Dar es Salaam.

Katika makubalino hayo, pande zote mbili zimekubaliana kufanya jitihada za dhati za kuimarisha ushirikiano huo kwa kuacha urasimu, kutojihusisha na vitendo vya rushwa, kuwa wawajibikaji zaidi na kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita kuwa na Tanzania ya viwanda.

Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto, amesema ushirikiano uliopo baina ya miji hiyo miwili unatakiwa kudumishwa na kuendelezwa kwa sababu unaleta umoja katika taifa.

Amesema kama viongozi wanaendelea kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan katika kutangaza nchi kimataifa pia kujenga uchumi.

"Tunapowakaribisha wageni kuja nchini watakuja na fedha watazitumia katika mambo mbalimbali hiyo itatusaidia kuongeza mapato ya ndani na wafanyabiashara kufanya biashara na kujiongezea kipato,"alisema na kuongeza:

"Haya ndio matunda ya Royal Tour imefanya wageni kuja na faida kubwa ni kupata mapato ya ndani kutokana na utalii, pato linakuja linaongezeka na linasaidia kutatua changamoto za wananchi, "amesema Kumbilamoto.

Amesema Rais Samia ameona utalii ni chanzo kipya cha kuongeza mapato katika nchi, wageni wanakuja nchini na kufanya nchi kufunguka na kuongeza mapato.

Kwa Upande Ofisa Mkazi Mji wa Hamburg jijini Dar es Salaam, Jinken Bruns amesema wataendeleza ushirikiano na Jiji la Dar es Salaam katika mambo mbalimbali.

Amesema ushirikiano huo waliosaini leo utalenga katika sekta mbalimbali, ambapo itasaidia kukuza uchumi na kuongeza mapato.

"Tunaadhimisha miaka 12 ya ushirikiano wetu baina ya Jiji la Dar es Salaam na Hamburg na urafiki huu utaendelea kuimarika siku zote katika kusaidiana mambo mbalimbali,"amesema

Naye Mwenyekiti wa wadau wa ushirikiano mji wa Dar es Salaam,  Michael Onesmo amesema uhusiano huo utakwenda kuinua mapato ya jiji na kuongeza ajira hasa kwa vijana.

"Moja ya manufaa ya mahusiano haya kati ya jiji la Dar es Salaam na Hambury yatakwenda kuboresha uchuni wetu kwa kuongeza mapato ya jiji na kuongeza  cha ajira," amesema.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/1e87e9594b2587f5294c735c069693fc.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi