loader
Mayele, Bangala, Inonga wawania Mchezaji Bora

Mayele, Bangala, Inonga wawania Mchezaji Bora

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Mayele, kiungo wa timu hiyo, Yanick Bangala na beki wa Simba, Henock Inonga ndiyo watakaowania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara katika sherehe zitakazofanyika Julai 7 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Bodi ya Ligi Kuu nchini (TPLB), imeeleza kuwa sherehe hizo zitafanyika ukumbi wa Rotana Hotel.

“Tuzo za TFF zimegawanyika katika makundi mbalimbali, zikiwemo Tuzo za Kikanuni za mashindano, Tuzo Binafsi za wachezaji na waamuzi, Tuzo za Heshima na Tuzo za Kiutawala zikihusisha wasimamizi wa mpira wa miguu na wadau wengine waliotoa mchango wao kwa mchezo huo.

“Ukiachana na tuzo za kawaida zinazohusiana na mashindano kwa maana ya bingwa, mshindi wa pili, mshindi wa tatu na wa nne, kutakuwa na tuzo binafsi 57, zikiwemo zile zinazotolewa kwa mtu zaidi ya mmoja, mfano Seti Bora ya Waamuzi, Kikosi Bora cha Ligi Kuu ya Wanawake na Kikosi Bora cha Ligi Kuu ya NBC,” imesema taarifa hiyo.

Orodha kamili ya tuzo hizo ni kama ifuatavyo: Mfungaji Bora Kombe la ASFC, Abdul Seleman (Coastal) goli 6, Heritier Makambo (Yanga) goli 3, Mfungaji Bora Ligi Kuu ya Wanawake, Asha Djafar wa Simba goli 27, mfungaji Bora Ligi Kuu, George Mpole wa Geita Gold goli 17.

Tuzo ya Timu yenye Nidhamu Ligi Kuu ya Wanawake inawaniwa na Yanga Princess,JKT Queens na Alliance Girls, wakati kwa Ligi Kuu ya NBC ni Prisons, Yanga na Simba, huku Meneja Bora wa Uwanja inawaniwa na Sikitu Kilakala  (Uwanja wa Azam Complex DSM), Mwaluka Modestus (Uwanja wa Sokoine Mbeya) na Godfrey Komba (Uwanja wa Manungu – Morogoro).

Tuzo ya Kamishina Bora Ligi Kuu ni Abousufian Sillia, Abubakary Kazinja na Somoe Ng'itu, huku Seti Bora ya Waamuzi ni mechi ya Yanga vs Simba, Mtibwa v Yanga na pia  Simba v Yanga.

Tuzo ya Mwamuzi Msaidizi Bora Ligi ya Wanawake inawaniwa na Zawadi Yusuph, Sikudhan Mkulungwa  na Glory Tesha, wakati Mwamuzi Msaidizi Bora NBC ni  Frank Komba, Mohammed Mkono na Janeth Balama.

Tuzo ya Kocha Bora Ligi ya Wanawake ni  Sebastian Nkoma,Simba ,Masoud Juma, Fountain Gate Princess na   Edna Lema - Yanga Princess, wakati Ligi Kuu ya NBC ni Nasredeen Nabi, Yanga, Fredy Minziro ,Geita na Juma Mgunda, Coastal.

Wanaowania Tuzo ya Chipukizi kwa wanawake ni Clara Luvanga,Yanga Princess, Frida Gerald, Fountain Gate na Winfrida Charles, Alliance, wakati kwa Ligi Kuu ni Dickson Mhilu, Kagera Sugar, Tepsie Evance, Azam na Richardson Ng'ondya, Mbeya City.

Tuzo ya Mwamuzi Bora wanawake inawaniwa na Tatu Malogo, Amina Kyando na Esther Adabert . Mwamuzi Bora Ligi Kuu NBC wanaowania ni Ramadhan Kayoko, Ahmed Arajiga  na Elly Sasii.

Wanaowania Tuzo ya Golikipa Bora ASFC  ni   Mohamed Mohamed ,Coastal, Djigui Diara, Yanga na Beno Kakolanya,Simba, wakati kwa wanawake ni Gelwa Yona, Simba, Asha Mrisho, Tiger na Caroline Rufa,  Fountain Gate, huku Ligi Kuu NBC ni Djigui Diara ,Yanga, Aishi Manula, Simba na  Khomein Abubakar, Geita.

Wanaowania Tuzo ya Beki Bora Ligi Kuu ni Djuma Shaaban, Yanga, Henock Inonga,Simba na Bakari Mwamnyeto,Yanga, wakati  Kiungo Bora ni Yanick Bangala ,Yanga, Feisal Salum,Yanga na Salum Abubakary, Yanga

Tuzo ya Mchezaji Bora ASFC wanaowania ni Abdul Selemani, Coastal, Feisal Salum,Yanga na Fiston Mayele,Yanga, wakati Mchezaji Bora wanawake wanaowania ni Asha Djafar,Simba, Amina Billal,Yanga na Fatma Issa Maonyo,Simba, huku Mchezaji Bora NBC wanaowania ni Mayele, Bangala (Yanga) na Inonga (Simba).

Wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora Championship ni Edward Songo-JKT Ruvu,Kenani Mwelukilwa-Kitayosa na Mohamed Haji Hamis,Mashujaa, huku wanaowania Mchezaji Bora First League ni Selemani Kibuta-Alliance, Mohamed Hussein-Copco Veteran na Yassin Mohamed Mgaza,Mbuni.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/1e782472d03e01ddba9d84156e9b6699.jpg

SIMBA Queens imekuwa timu ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi