loader
Pacha walioungana watenganishwa Muhimbili

Pacha walioungana watenganishwa Muhimbili

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam, leo imefanikiwa kuwatenganisha watoto pacha Neema na Rehema  wenye umri wa miezi tisa, waliozaliwa wakiwa wameungana sehemu ya kifua, tumbo na  ndani wameungana ini huku kila mtoto akiwa na ini lake.

Upasuaji huo umechukua saa saba kwa ushirikiano wa  jopo la madaktari bingwa wa upasuaji watoto, upasuaji viungo watoto, upasuaji ini, plastic surgery, wataalamu wa dawa za usingizi, wataalamu wa uangalizi maalumu (Intensivist), wataalamu wa radiologia, wauguzi, na wataalamu wa maabara.

Hatua hiyo imeifanya Tanzania kuwa nchi ya tatu Afrika kufanya upasuaji huo baada ya Afrika Kusini na Misri.

Upasuaji kama huo ni mara ya tatu kufanyika hapa nchini ambapo mara ya kwanza ulifanyika mwaka 1994, ukihusisha watoto wawili wa kiume waliokuwa wameungana kwenye tumbo.

Upasuaji wa pili ulifanyika mwaka 2018, ukihusisha watoto wawili wa kiume wanaoishi Kisarawe, ambao wana  miaka mitatu na miezi tisa sasa na wanaendelea vizuri.

Daktari Bingwa Mshauri Mwelekezi-Upasuaji wa Watoto, Petronila Ngiloi, alisema watoto hao walizaliwa  Septemba 21, 2021 kwa njia ya upasuaji wakiwa na kilo 4.9 wote kwa pamoja katika Hospitali ya Wilaya ya Maswa, Mkoani Simiyu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c0d76504a55d0e7e37405f7d73c95416.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Aveline Kitomary

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi