loader
CRDB, wakala waja na mwarobaini ukusanyaji mapato Z’bar

CRDB, wakala waja na mwarobaini ukusanyaji mapato Z’bar

BENKI ya CRDB imeingia makubaliano na Wakala wa Serikali-Mtandao visiwani Zanzibar (E-Government) yatakayorahisisha SMZ utoaji huduma kwa wananchi pamoja na ukusanyaji wa mapato.

Katika hafla ya kusaini makubaliano hayo yaliyofanyika Hoteli ya Park Hyatt, Unguja, Zanzibar leo, CRDB iliwakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Abdulmajid Nsekela huku Wakala wa  Serikali Mtandao Zanzibar (E-Government ) ukiwakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji, Said Seif Said

Imeelezwa kuwa makubaliano hayo yanatarajiwa na kusaidia ukuaji wa utalii kwa kuwa na kituo kimoja cha makusanyo (one centre collection).

Mbali na wakuu hao wa CRDB na wakala, maofisa mbalimbali kutoka benki hiyo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) walihudhuria tukio hilo.

 

 

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/57fe2d80cfa9f8376002fdda5e5d6a70.JPG

UKOSEFU wa elimu ya biashara, uthubutu na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi