loader
Samia aagiza Sports Arena zijengwe Dar, Dodoma

Samia aagiza Sports Arena zijengwe Dar, Dodoma

RAIS Samia Suluhu Hassan, amewapongeza wachezaji na timu zilizofanya vizuri katika mashindano ya kimataifa, huku akiagiza Sports Arena kujengwa Tanganyika Packers, Dar es Salaam na Sabasaba, Dodoma.

Amesema hayo leo Julai 5, 2022, Ikulu Dar es Salaa,  alipokutana na wachezaji na benchi la ufundi la timu ya taifa ya wasichana umri chini ya miaka 17 ya Serengeti Girls na kula nao chakula cha mchana.

Alisema anaipongeza Serengeti Girls, timu ya taifa ya soka la walemavu ya Tembo Warriors pamoja na wanariadha Alphonce Simbu na wengine, ambao wamefanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Serengeti Girls imefuzu fainali za Kombe la Dunia kwa umri huo, ambazo zitafanyika India kuanzia Oktoba 11 hadi 30, 2022 wakati Tembo Warriors nao watacheza fainali za Kombe la Dunia Istanbul, Uturuki Oktoba mwaka huu.

Akizungumzia Sports Arena, Samia aliagiza kwa Dar es Salaam uwanja huo ujengwe eneo la Tanganyika Packers kwa kuwa ni eneo ambalo linafikika kirahisi na ni njia mojawapo ya kueneza michezo katika maeneo tofauti ya Dar es Salaam.

Alisema uwanja huo usijengwe karibu na vilipo viwanja vya Uhuru na kile cha Benjamin Mkapa, huku Arena ya Dodoma ijengwe eneo la Sabasaba.

"Wizara ya Michezo na Wizara ya Ardhi mkutane muangalie umiliki wa eneo la Tanganyika Packers, najua una utata unaweza umalizwe ili eneo hilo ligengwe arena maana ni rahisi kufikika kirahisi," alisema.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa alitaka serikali kukubali Tanzania kuwa mwenyeji wa fainali za Michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wanawake mwaka 2024 na zile za wanaume, Afcon mwaka 2027 na kumuomba Rais kuridhia maana ameifungua nchi kupitia Royal Tour sasa ni wakati wa michezo kufanya hivyo.

Alisema Tanzania imejipanga kwa ajili ya kuwa mwenyeji, lakini lazima sapoti ya serikali iwepo.

Naye Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia alimshukuru Rais Samia kwa Serikali kugharamia mkutano mkuu wa CAF kwa asilimia 100, kwani wenyewe wangeelemewa.

Pia alimuomba serikali kusamehe deni la TRA linalotokana na Brazil kufanya ziara ya soka Tanzania, ambapo katika deni hilo tayari wamelipa kiasi cha Sh bilioni 5 na hakusema bado wanadaiwa kiasi gani.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8e66d78ca10589c525248b2b376cd07d.jpg

SIMBA Queens imekuwa timu ya ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi