loader
Serikali yaahidi ushirikiano vita ya Uviko 19

Serikali yaahidi ushirikiano vita ya Uviko 19

MAKAMU wa Rais Dk. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambaye ni Mratibu wa Mpango wa Ushirikiano katika Usambazaji wa Chanjo ya Uviko19, Ted Chaiban, mazungumzo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amesema Serikali imelenga kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kukabiliana na Uviko 19, ikiwemo kutoa chanjo hususani kwa watu wote walio katika hatari ya kupata madhara zaidi ya ugonjwa huo.

Amesema kudhibiti ugonjwa huo, Tanzania imeendelea kuimarisha mifumo ya afya, kuwajengea uwezo watumishi wa afya katika kukabiliana na ugonjwa huo, kuimarisha huduma za dharura pamoja na ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya, ili kusaidia huduma muhimu ya afya, ambayo iliathiriwa na janga la Uviko-19 hususani kwa huduma ya afya ya msingi.

Ameongeza kwamba pamoja na mafaniko yaliyopatikana katika kudhibiti Uviko-19, bado serikali inaendelea kuchukua hatua muhimu katika kukabiliana na ugonjwa huo, ikiwa ni pamoja na  kujenga miundombinu itakayoweza kukabiliana na magonjwa ya mlipuko pindi yatakapotokea.

Kwa upande wake Chaiban, ameipongeza Tanzania kwa juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya utoaji wa chanjo.

Amesema ofisi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuwafikia watu wengi zaidi wanaohitajika kupata chanjo ikiwemo makundi maalum, kama vile watumishi wa afya pamoja na wazee.

Amesema juhudi za ufanikishaji wa utoaji chanjo zinapaswa kuhusisha moja kwa moja ngazi ya mikoa na wilaya, ili kufikia kirahisi malengo ya taifa katika zoezi hilo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c77f4161b5191e0280c8efd4836a6ea1.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi