loader
Waziri asitisha mkataba uwekezaji shambani

Waziri asitisha mkataba uwekezaji shambani

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula amezuia mkataba wa upangishaji ardhi wa mashamba matatu maarufu kama mashamba ya Steyn yaliyopo wilayani Monduli mkoani Arusha ulioingiwa kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Monduli na kampuni ya EBN Hunting Safaris.

Halmashauri ya Wilaya ya Monduli ilisaini mkataba wa uwekezaji kwenye mashamba hayo ulioibua mkanganyiko baina ya Ofisi ya Msajili wa Hazina na halmashauri hiyo.

Halmashauri hiyo ilitafuta mwekezaji kwenye mashamba hayo baada ya kufutwa na Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa kupitia tangazo la serikali la mwaka 2005 kwa lengo la upanuzi wa mji wa Makuyuni.  

Mashamba ya Steyn ni muunganiko wa mashamba matatu ya Lente estate, Amani na Loldebes yenye ukubwa wa ekari 15,163 yaliyopo wilayani Monduli.

Inaelezwa katika kipindi cha miaka ya 1970, raia waliomiliki mashamba hayo waliondoka nchini na kuyaacha yakimilikiwa na Hermanus Steyn kupitia kampuni ya Rift Valley Seed Company Ltd. 

Dk Mabula alisema mashamba hayo kwa mujibu wa sheria ya masuala ya utwaaji yako chini ya umiliki wa Msajili wa Hazina hivyo uongozi wa Wilaya ya Monduli ulitakiwa kuomba kibali cha matumizi ya eneo baada ya kutwaliwa.

 'Kuanzia sasa halmashaur itambue eneo hili litakuwa chini ya usimamizi wa Maliasili na Utalii na wamewapa Tawa kwa ajili ya kuona namna ya kuliendesha,'' alisema. 

Awali, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Isack Joseph katika kikao cha ndani alimueleza Dk Mabula kuwa, halmashauri hiyo ilisaini mkataba wa kukodisha mashamba hayo kwa mwekezaji kwa kuwa haina chanzo cha mapato cha uhakika.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8abcacde359560e02191eece8f4ac14a.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Monduli

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi