loader
Ummy: Covid-19 bado  ipo, chukueni tahadhari

Ummy: Covid-19 bado ipo, chukueni tahadhari

WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Watanzania wanapaswa kuendelea kuchukua tahadhari kuepuka kuambukizwa virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19 kwani bado ni tishio nchini kutokana na kasi ndogo ya kuchanja.

Alisema hayo jana wakati wa ufunguzi wa majengo ya afya ya mama na mtoto katika Hospitali ya CCBRT, mkoani Dar es Salaam.

Alisema anapata tabu kuruhusu wananchi waache kuvaa barakoa kwa kuwa takwimu zinazoendelea kuifikia wizara yake zinaonesha idadi ya wagonjwa inazidi kuongezeka.

Alisema wiki hii maambukizi zaidi yameripotiwa na asilimia kubwa ni kutoka Mkoa wa Dar es Salaam.

“Kuna maswali watu wengi wananiuliza kuhusu barakoa wakishangaa kwa nini wazungu hawavai huku Watanzania wakisisitizwa kuendelea kuzivaa.”

“Wale hawavai barakoa kwa kuwa wamechanja hadi kufika wastani wa asilimia 70 ndio maana hawavai. Hata hapa kama tungechanja hadi kufika angalau asilimia 50, ningewatangazia watu wasivae barakoa, hivyo tuendelee kuchanja ili kufikia viwango vitakavyotuwezesha kuacha barakoa,” alisema Ummy.

Mlezi wa Hospitali ya CCBRT Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukubali jengo hilo lipewe jina lake.

Balozi wa Ujerumani nchini, Regine Hess alisema serikali ya nchi hiyo ilichangia Euro milioni 18.5 katika ujenzi wa jengo hilo na akamshukuru Rais Samia kwa kuwa kielelezo cha kupatikana kwa usawa wa kijinsia nchini.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/b6623581d7e49f86c4110eab43d6e957.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Selemani Nzaro

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi