loader
Maeneo mapya utalii yazidi kufunguka

Maeneo mapya utalii yazidi kufunguka

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema fedha za Covid-19 zimesaidia kufungua maeneo mapya ya utawala ikiwamo Pori la Akiba la Mkungumero.

Masanja amayasema hayo wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Bajeti iliyokagua miradi inayotekelezwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).

 "Fedha za Covid -19 zimetusaidia kufungua maeneo mengine mapya ya utalii ambayo yatasaidia kuongeza watalii ambao wataweza kutembelea maeneo yetu yaliyohifadhiwa," amesema na kuongeza:

“Baada ya uzinduzi wa Royal Tour, tulikuwa na wasiwasi wageni tutawapeleka wapi wakijaa Serengeti, Ngorongoro na maeneo mengine muhimu ambayo watalii wanapenda kutembelea.

“Ujio wa fedha za Covid-19 zimetusaidia kupanua wigo wa maeneo ya kutembelewa,” amesema Naibu Waziri huyo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/3bb4e757bb065ba2c8d7667d384065ab.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi