loader
Kamati ya Bunge yaipongeza TAWA

Kamati ya Bunge yaipongeza TAWA

KAMATI ya Bunge ya Bajeti imeridhishwa na kupongeza utekelezaji wa miradi ya miundombinu inayotekelezwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).

Miradi hii ni ile inayotekelezwa kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Covid 19, ambapo TAWA ilipelekewa Sh bilioni 12 kati ya Sh bilioni 90.2 zilizoelekezwa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Akizungumza baada ya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi hiyo katika Pori la Akiba la Mkungunero ambapo limepelekewa Sh milioni 672, Mwenyekiti wa Kamati, Daniel Sillo alisema kazi iliyofanyika ni ya kuridhisha.

" Kwanza tumpongeze Rais Samia kutafuta fedha kwa ajili ya elimu, afya na sekta ya utalii, ambayo inafungua fursa kubwa kwa taifa letu, pia niipongeze wizara kwa ajili ya usimamizi mzuri wa fedha za umma.

 

 

 " Nichukue nafasi hii kwa niaba ya wajumbe wa kamati kwa kazi hii nzuri ambayo tumeishuhudia kwa macho yetu kwa kweli mnastahili pongezi, hatua hizi zinafungua fursa ya utalii hapa nchini na sisi wote tunajua mheshimiwa Rais Samia amefungua njia kwa filamu ya Royal Tour, ambapo tunashuhudia kwa sasa hoteli nyingi zimejaa, tunampongeza  sana Rais,”

Amesema kwa sasa sekta ya utalii inachangia takribani asilimia 17 ya pato la taifa na asilimi 25 ya fedha za kigeni na kuwa maboresho yanayofanywa yataongeza mchango wa sekta.

"Maboresho haya tunayoyafanya Mkungunero na maeneo mengine yote yataaongeza uchangiaji kwenye pato la taifa, kwa hiyo endeleeni na kusimamia miradi hii yenye manufaa kwa taifa letu niwaombe kusimamia vizuri fedha za umma ili zilete tija kwa Watanzania wa leo na vizazi vijavyo," amesema.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema uboreshaji wa miundombinu katika Pori la Akiba Mkungunero utatoa wigo mpana wa eneo hili kutembelewa na watalii kwa sababu ya miundombinu inayoendelea kuwekwa. 

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara  ya Maliasili na utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka, aliipongeza TAWA kwa nzuri na aliishukuru kamati kwa kutenga muda kwa ajili ya kupitia miradi hiyo.

Naye Kaimu Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Mlage Kabange alimshukuru, Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizi ambazo zimetolewa kwa kipindi muafaka wakati Taifa likijiandaa kupokea wageni wengi baada ya uzinduzi wa filamu Royal Tour.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/0c66e46ba37d68ddace754b6babb0f49.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi:  Anastazia Anyimike, Kondoa

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi