loader
Pacha waliotenganishwa wazidi kuimarika

Pacha waliotenganishwa wazidi kuimarika

PACHA Rehema na Neema waliotenganishwa Julai mosi, 2022 katika Hospital ya Taifa Muhimbili hali zao zinaendelea kuimarika.

Pia Wizara ya Afya, imesema itaweka mkakati endelevu wa kuwafuatilia watoto hao kujua hali zao pamoja na kutoa msaada kwa familia.

 

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu aliyasema hayo leo  alipowatembelea ili kuwajulia hali.

 

Waziri Ummy amefurahishwa na hali za maendeleo ya kiafya ya watoto hao kuendelea vizuri na kuwapongeza jopo la madaktari kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na madaktari kutoka Bahrain.

 

“Wataalamu wetu wamefanya upasuaji wa kuwatenganisha kwa mafanikio makubwa, nimefurahi kuona watoto wanaendela vizuri, wamenieleza upasuaji huu ni mgumu sana, leo ni siku ya nne na Watoto wanaendelea vizuri tunamshukuru Mungu,” amesema Waziri Ummy.

 

Amesema katika mwaka huu mpya wa bajeti 2022/23 Serikali imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 8 kwa ajili ya mafunzo kwa madaktari, ili waweze kuongeza ujuzi na kuweza kutoa huduma za kibingwa hapa nchini.

“Tunao wajibu wa kuweka rasilimali fedha kwa ajili ya mafunzo kwa watumishi, vifaatiba pamoja na dawa na miundombinu, tutaendelea kuweka fedha kwa ajili ya mafunzo kwa madaktari bingwa na bingwa bobezi,” amesema Waziri Ummy.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/104454633b9904cba26aa57fb8a1f4a5.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Aveline Kitomary

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi