loader
RC Tanga ataka wataalamu wasitumike kisiasa

RC Tanga ataka wataalamu wasitumike kisiasa

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima amewataka wataalamu kuacha kutumika kisiasa na kusababisha kutekeleza miradi ambayo haileti tija kwa wananchi, huku serikali ikipoteza fedha nyingi.                   

Ushauri huo ameutoa wakati wa ziara yake ya kukagua jengo la kituo cha kuhifadhi nafaka na mbogamboga katika eneo la Malindi wilayani Lushoto.

Amesema kuwa serikali imefanya uwekezaji wa jengo lenye thamani ya Sh Bil 1.8, lakini limeshindwa kuleta tija kutokana na wakulima kushindwa kufika kwenye eneo hilo.

"Jengo hili wataalamu mmetupiga change la macho, kwani halijaweza kukidhi malengo na matakwa ya serikali kumsaidia mkulima kiuchumi, bali kumuongezea shida ya kuendelea kuhangaika kutafuta masoko ya mazao yake,"amesema RC Malima.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Kalist Lazaro, amesema dunia wanapigania upotevu wa chakula, lakini kwa Lushoto kwa uwekezaji wa soko hilo haujaweza kuleta tija.

Naye Ofisa Kilimo wa Wilaya hiyo Abdulkarim Kimbunga, amesema kuwa kuanzishwa kwa soko hilo kulilenga kupunguza upotevu mazao baada ya kuvunwa, hususani matunda na mbogamboga.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d1a82b969971860cdf16ec74bd285851.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Amina Omary, Lushoto

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi