loader
Serikali yakabidhiwa ng'ombe boran

Serikali yakabidhiwa ng'ombe boran

MKURUGENZI wa Ranchi ya Mbogo, Mbogo Pirmohamed Mulla, amekabidhi Ng’ombe dume aina ya Boran kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki  kwa kumkabidhi nyaraka ya umiliki wa ng’ombe huyo.

Katika taarifa yake, Mulla amesema, wameamua kutoa msaada kwa serikali ili atumike kuzalisha mbegu na kupandikizwa kwa ng’ombe jike na  kuboresha hali ya mifugo nchini. 

Amesema ng’ombe huyo ana umri wa mitatu akiwa na  kilogramu 624 na ana thamani ya Shilingi Milioni 6.

Kwa upande wa Waziri Ndaki amesema dhamira ya serikali ni kuhimilisha ng’ombe jike laki tatu kwa mwaka wa fedha 2022/23, hivyo ng’ombe huyo atapelekwa katika Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji kilichopo jijini Arusha kwa ajili ya kuzalisha mbegu. 

Makabidhiano hayo yamefanyia katika viwanja vya John Mwakangale yanapofanyika Maonesho ya Wakulima Nanenane kitaifa jijini Mbeya.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/cc15d294b2a4fe35990753500718a2f2.PNG

MKE wa mmoja wa watu 20 waliokufa kwenye ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi