loader
Vituo vitano kujengwa kuibua ubunifu nchini

Vituo vitano kujengwa kuibua ubunifu nchini

TUME ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari itajenga vituo vitano nchini kwa lengo la kuibua ubunifu. Akizungumza jijini hapa, Mkurugenzi Mkuu wa Tume, Dk Nkundwe Mwasaga alisema miongoni mwa vituo hivyo ni pamoja na cha Dodoma kitakachokwenda sambamba na ujenzi wa chuo kikubwa cha Tehama.

“Mpango huo wa tume umewezeshwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari katika mwaka huu wa fedha 2022/2023,” alisema. Alisema vituo hivyo vitajengwa pia Mwanza kwa upande wa Kanda ya Ziwa, Arusha katika Kanda ya Kaskazini, Dar es Salaam katika Kanda ya Mashariki na Mbeya katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Vituo hivyo vitakuwa na kazi ya kuibua ubunifu ili kampuni ndogondogo katika maeneo hayo zitengeneze bidhaa za ubunifu na kuzisambaza katika maeneo mengine. Dk Mwasaga alisema katika kuhakikisha nchi inajikita katika uchumi wa kidijiti, tume imeweka mkakati kutekeleza mambo matano ili kuwa kama India inayojiendesha kwa kutumia uchumi huo.

Mambo hayo ni pamoja na kuhakikisha shughuli nyingi za Watanzania zinafanyika kupitia mtandao na tume itakuwa makini kuhakikisha mifumo hiyo inabaki salama wakati wote

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5f7b7a813d4d831c955d423c187cf344.jpeg

MKUU wa Wilaya ya Kilombero, mkoani ...

foto
Mwandishi: MAGNUS MAHENGE, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi