loader
Samia atoa agizo maeneo ya utawala

Samia atoa agizo maeneo ya utawala

RAIS Samia Suluhu Hassan, amezuia maeneo yote nchi nzima kupandishwa hadhi au kukatwa kwa ajili ya maeneo mapya ya utawala.

Agizo hilo amelitoa leo Agosti 10, 2022 mkoani Njombe, baada ya wakazi wa Mkoa huo kumuomba Njombe ipandishwe hadhi na kuwa manispaa.

Rais Samia amesema kupandishwa hadhi, maeneo au kutengwa maeneo mapya ya utawala kuendane na hali ya uchumi, ambayo kwa sasa hauruhusu kufanya, hivyo kwani itakuwa mzigo mkubwa kwa serikali.

“Kila ninapopita watu wanaomba kupandishwa hadhi au kukatiwa maeneo ya utawala, lakini kwa hali yetu ya uchumi ni mzigo mkubwa, tuna mzigo mkubwa wa huduma kwa wananchi unaotukabili, huduma za afya, umeme, barabara, madarasa, ” amesema na kuongeza:

“Kwa sasa twende kama tulivyo, mwelekeo ni kilimo, mwelekeo ni kuinua uchumi,” amesema.

Akizungumzia ombi la wazee wa Mkoa wa Njombe, kumuomba kuwa mlezi Rais Samia amesema: “Niliongea na wazee wakaniomba niwe mlezi,  ulezi upo aina mbili Chama Cha Mapinduzi, kuna walezi kila mkoa, serikali hakuna walezi, Rais ni mlezi wa Tanzania yote, sio kwamba nakataa lakini siwezi kupendelea mtoto mmoja kati ya watoto 26.”

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/6f7bc533bcb78a5c14d9420a31de0fc7.jpg

SERIKALI inatekeleza mradi wa maji wenye thamani ya ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi