loader
Dstv Habarileo  Mobile
AGRA yaridhika na Serikali kuinua kilimo

AGRA yaridhika na Serikali kuinua kilimo

Hivi karibuni Rais Kikwete alisema kwamba Serikali yake ipo karibu na kufikia Malengo ya Azimio la Maputo la kilimo na usalama wa chakula, ambapo inatakiwa asilimia 10 ya pato la Taifa kutumika katika kilimo.

Pamoja na kukubali kwamba Serikali imepiga hatua katika utekelezaji wa azimio hilo, amesema Serikali yake itaendelea kuchukua hatua zaidi.

Kauli hiyo ya Rais imetolewa katika hotuba yake aliyoitoa kwenye kampeni ya Afrika Moja yenye kusema Kilimo kinalipa ambapo wasanii wa Bongo Fleva waliwasilisha kauli ya wakulima wadogo wapatao milioni 2 ambao wanataka Serikali kufanya zaidi ili wawe na soko la uhakika.

Wasanii hao mashuhuri Diamond Platnumz, Mrisho Mpoto na Ambwene Yessayah (AY), waliwasilisha saini za wakulima hao, wakati Serikali imesema kutakuwa na mavuno makubwa.

Pamoja na kusema mavuno yatakuwa mengi kutokana na ushirikiano uliopo wa sekta binafsi na umma, alisema zipo changamoto za soko.

Alisema ipo haja ya wadau wa sekta ya kilimo kuangalia namna ya kukabiliana na tatizo la soko.

Mwakilishi wa AGRA nchini Tanzania, Dk Mary Mgonja aliwaambia washiriki kwamba utafiti uliofanywa na Farm Radio International and Agriculture Non State Actors Forum (ANSAF), unaonesha kwamba ipo haja ya kuhakikisha kwamba kuna Menejimenti ya mavuno mengi yanayokuja inakuwapo.

Pia, ipo changamoto ya wakulima kuwa na masoko yanayowapa ushirikiano mkubwa na bei nzuri.

Katika mazungumzo ilielezwa kuwa wakulima walikuwa hawanufaiki na ugunduzi na uvumbuzi unaofanywa na wataalamu wa kilimo.

Dk Mgonja alisema kwamba wingi wa taarifa zenye kuwafaa wakulima ni bidhaa adimu lakini inatakiwa ugunduzi kuwafikia ili waweze kubadilika.

Alisema kwamba AGRA na wadau wengine miaka michache iliyopita, wamejiwekeza zaidi katika utafiti ambapo matokeo mazuri yanawezesha baadhi ya mazao yaliyokuwa katika hali mbaya kurejeshewa matumaini.

Tafiti hizi zimesaidia mathalani kurejesha kilimo cha muhogo visiwani Zanzibar. Alisema kutokana na utafiti huo, Zanzibar imeendelea kulima muhogo, kutokana na mbegu mpya kuwa na uwezo wa kukabiliana na maradhi.

Mbegu mpya inayolimwa sasa ni Kizimbani na Mahonda. Dk Mgonja alisema kwa kushea utafiti kunawezesha wakulima wadogo kuwa na mabadiliko makubwa.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi