loader
Ahmadiyya yasaidia vyakula wajane 80

Ahmadiyya yasaidia vyakula wajane 80

Akizungumza kwenye hafla ya kutoa misaada hiyo, Shehe wa Mkoa wa Dodoma na Singida, Bashart Rehman Butt alisema msaada huo umelenga katika kuwasaidia wajane hao kwenye Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Misaada hiyo ni mchele, sukari na maharage. Kiongozi huyo wa Ahmadiyya alisema taasisi yake imelazimika kuwasaidia wajane hao kutokana na jamii imekuwa ikisahaulika jambo ambalo limekuwa likileta kero katika kupata mahitaji yao kwa kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Aidha Shehe huyo amezishauri taasisi, madhehebu ya dini na watu binafsi kuelekeza misaada yao kwa watu wenye mahitaji mbalimbali ili waweze kupunguza ukali wa maisha yao wanayokutana nayo kila siku.

Kwa upande wake mjane Hadija Mwinyiam ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Samora Air Port Kata ya Viwandani, akizungumza kwa niaba ya wajane hao amezitaka taasisi nyingine kutumia fursa walizonazo kwa kuzisaidia jamii zenye mahitaji muhimu.

Alisema kuna jamii nyingi zikiwemo yatima, wajane, wazee wasiojiweza na wale wanaoishi katika mazingira magumu, zimekuwa zikitaabika kwa kukosa mahitaji muhimu ikiwemo elimu, afya, mavazi na hata kwa chakula.

Diwani wa Kata ya Viwandani, Jafari Mwanyemba akizungumza na wajane kwenye hafla hiyo, aliwataka wajane hao kutumia msaada huo kwa malengo maalumu na siyo vinginevyo.

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi