loader
Dstv Habarileo  Mobile
Al Shabaab waua watu 10 Kenya

Al Shabaab waua watu 10 Kenya

Shambulizi la jana, linalosadikiwa kufanywa na kundi la wanamgambo wa Al Shabaab, liliteketeza watu 48 katika eneo la Mpeketoni karibu na Mji wa Lamu.

Shambulizi lingine lilitokea leo katika eneo hilo, lililoko pwani ya Kenya na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 10.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi hiyo, Joseph ole Lenku, washambuliaji waliharibu kituo cha mawasiliano cha Safaricom, kabla ya kutekeleza uhalifu huo, wakilenga kuzuia wakazi kuwasiliana na watu wa nje.

Polisi nchini Kenya walisema, washambuliaji hao walitekeleza uhalifu huo usiku kucha, wakifyatua risasi hovyo kwa wananchi, ambao wengi wao walikuwa wakiangalia mechi ya Kombe la Dunia.

Taarifa zilisema kundi la Al Shabaab, lilikiri kufanya mashambulizi hayo na lilisema kuwa operesheni yao ya mashambulizi, itaendelea nchini Kenya.

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi