loader
Dstv Habarileo  Mobile
Ali Kiba arejea na mbili mpya

Ali Kiba arejea na mbili mpya

Akizungumza mwishoni mwa wiki baada ya kutembelea ofisi za gazeti hili Tazara, Dar es Salaam, Kiba alisema mashabiki wake wamekuwa wakimtaka kuleta burudani kwani alikaa kwa takribani miaka kama miwili bila kutoa wimbo wowote.

“Kwa kipindi nilichokaa kimya nilikuwa kama shabiki wa muziki wa watu wengine, na mashabiki wangu walikuwa wakiniulizia mbona sirudi, sasa nimerudi nitaendelea kuwaletea burudani kali kama zamani,” alisema Kiba.

Kiba aliyekuwa akifanya vizuri ndani na nje ya nchi na nyimbo zake za Cinderella, Mapenzi Yanarun Dunia, My everything na Dushelele, alisema sasa hakuna kulala tena, amejipanga kuendelea kutoa vitu vikali.

“Unajua mashabiki wangu, marafiki na wadau wameniomba nisikae tena muda mrefu, ndio maana kwa kurudi nikaachia mbili kwanza, huku nikiendelea kuwaletea nyingine kali zitakazotamba kimataifa,” alisema.

Katika wimbo wa Kimasomaso, ameimba ‘remix’ ya wimbo wa marehemu Issa Matona aliyeuimba katika mahadhi ya taarabu, wakati yeye ameuimba kisasa ili kuwavutia mashabiki wake ndani na nje ya nchi.

Alisema sababu kubwa ya kuchukua wimbo huo ni kujaribu kurudisha muziki wa kizamani katika ladha tofauti ilimradi mashabiki wake wafurahie na kuburudika.

Tangu ameanza muziki, wimbo wake wa Cinderella ndio uliomwekea rekodi kwa kuuza nakala nyingi Afrika Mashariki mwaka 2008. Mwaka 2012, alishinda Tuzo ya Wimbo Bora wa Zouk kupitia wimbo wake wa Dushelele katika Tuzo za Muziki za Kilimanjaro.

YANGA leo saa 1:00 usiku itashuka dimbani kuikabili ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi