loader
Ashauri namna ya kukwepesha hasara ya mishahara

Ashauri namna ya kukwepesha hasara ya mishahara

Hayo yalibainishwa jana na Mkaguzi Mkazi wa Mkoa wa Morogoro, Sylvester Kibona katika kikao maalum cha kujibu hoja za ukaguzi wa fedha za Serikali kilichofanyika wilayani humo.

Kibona alisema watumishi hao wanapaswa kuhakikisha majina hayo yanaondolewa kwenye orodha ya mishahara ili Serikali isiendelee kupata hasara kwa kuendelea kulipa mishahara hewa.

Aidha alisema halmashauri hiyo pia inakabiliwa na tatizo katika ukusanyaji mapato ambapo alisema kuwa kuna baadhi ya watu wanadaiwa kiasi kikubwa cha pesa. Hivyo aliwashauri kukusanya kwa kutumia sheria ambazo wamejiwekea.

Naye Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Emir Mubarack alisema wanahakikisha wanashirikiana vizuri na watendaji wa kata na idara japo huko nyuma madiwani walikuwa nao wanataka wawe kama watendaji na kwamba dosari hizo walishaziondoa.

Akizungumzia tatizo la ulipaji mishahara hewa Mwenyekiti huyo alisema kuwa hata wao wanashangaa kuona mishahara ya wastaafu na waliokufa bado inaingia wakati taarifa zao zilishapelekwa.Hata hivyo alisema wamejipanga kuhakikisha changamoto hizo hazijirudii tena.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Idd Mshili alisema pamoja na halmashauri hiyo kuwa kongwe pamoja na kuwa na fursa nyingi ikiwemo ya kuzalisha chakula kwa wingi na kutegemewa na nchi nzima kwa uzalishaji wa chakula lakini bado inakabiliwa na changamoto ya ukusanyaji wa mapato.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso ...

foto
Mwandishi: Agnes Haule, Kilosa

Post your comments